Jesus Filme

 MJUE "BRIAN DEACON" ALIYEIGIZA FILAMU YA YESU, FILAMU MAARUFU ZAIDI ULIMWENGUNI. 


Watu wengi ambao wametokea kuangalia sinema ya maisha ya Yesu, hupata taswira ya kiimani kwamba muingizaji huyu ni Yesu au kwa utamaduni wa utayarishaji wa sinema mbali mbali  kwamba hata kama sio Yesu alau walimtumia muigizaji anayemfanana.


Kwa upande mmoja sinema hii imeleta matokeo chanya kwa mamilioni ya watu na wengi wakibadili maisha yao na kumfuata Yesu. Hata hivo kila zuri halikosi changamoto yake. Baadhi hata anapokuwa kwenye maombi huvuta picha hii kana kwamba anamuona Yesu. 

Huyu sio Yesu bali kama nilivosema ni muigizaji au mcheza sinema jina lake anaitwa Brian Deacon ni mwingereza. Alizaliwa tarehe 13/02/1949 Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia. baba yake alikuwa fundi makanika na mama yake alikuwa Unesi.

Yesu hakuoa lakin huyu alikuwa na mke. Ndoa yake ya kwanza alimuoa Bi Rula Lenska ingawa waliachana baadae na akaoa mke mwingine huyu wa kwanza walifanikiwa  kumzaa binti Lara Deacon. Mke wa wake wa pili ni Bi Natalie Bloch aliyemuoa mwaka 1998.


Kama nilivosema, sinema hii sio tu wengi walio na wanaitizama inabadilisha maisha yao lakini yeye mwenyewe alipoiangalia baada ya kuicheza alimpa Yesu maisha yake, wakati huo akiwa na miaka 30.

Wakiwa wana andaa na kutafuta nani aigize kama Yesu ulipita mchujo mkali sana kutoka kwa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza (screen test) kuona kwamba wanafaa. Alikuwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael, waliovuka mchujo huu na kisha kuingia kwenye usaili maalumu. Yeye alitokea Kampuni ya New shakespears ambayo alikuwa akiifanyia kazi za Sanaa na uigizaji. 

Anadai kulikuwa na mengi yaliyo onekana ni magumu kama vile utulivu sirika na kuingiza upole na ujasiri wa Yesu.

 Alilazimika kusoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian anasema, walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa ‘mkristo jina’ wa kanisa katoliki, alikuwa ana uwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla. 

Siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto, lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa, shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake. 

haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia, baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu, ukweli na kugusa mioyo ya watu.

Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233 (kwa takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu, filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage. ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian mwenyewe hiwaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo, ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza, ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

Hata hivo huyu Bwana amewahi kucheza sinema nyingine mbali na sinema ya maisha ya Yesu ambazo ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

Sinema hii ilichezewa nchini Israeli.

Ikiigizwa na Bwana  Brian Deacon,

Muamdaaji wa makala hii ni Victor oredi 

Muasisi wa Amazon VIDEO library .



Comments

Popular Posts