Siri Kubwa kuhusu vita ya Vietnam

KATIKA VITA AMBAZO MAREKANI HAITAKAA ISAHAU KATIKA USO WADINIA NI VITA YA VIETNAM

Vita za Vietnam ni moja kati ya vita katika historia ya Marekani ambazo taifa kubwa na lenye nguvu duniani lililazimika kuondoka uwanja wa mapambano baada ya kushindwa vibaya.

Vita hizi zilipigwa kuanzia mwaka 1955 mpaka 1975, na zilipigwa maeneo ya Vietnam kwenyewe, Laos na Cambodia.


Kwa juu juu ilikuwa ni vita iliyopigwa kati ya Vietnam Kaskazini na Vietnam Kusini lakini nyuma ya pazia ilikuwa ni vita ya kijasusi kati ya wababe wa dunia wa wakati huo yaani Marekani na Urusi ya Kisovieti(proxy war), huku kila mbabe akitaka kupandikiza itikadi yake kwa upande huo, Marekani akitaka Ubepari utawale na Mrusi akitaka Ukomunisti utawale.


Vietnam ya Kaskazini ilisapotiwa na Urusi ya wakati huo(USSR), China na nchi nyingine za Kikomunisti huku Vietnam ya Kusini ikisapotiwa na Marekani, Korea Kusini, Australia, Thailand na nchi nyingine zilizokuwa zikipinga Ukomunisti.


Wakati vuguvugu la vita limeanza kukolea mwaka 1950 Marekani ilituma kikosi cha majasusi wake nchini Vietnam wakati huo ikiwa Koloni la Mfaransa ikijulikana kama French IndoChina kwa ajili ya mafunzo, udukuzi na kukusanya taarifa za kijasusi kabla ya kuanza mashambulizi mazito, lengo likiwa kutoa mafunzo ya kijeshi na kijasusi kwa askari wa Vietnam ya Kusini na kuviandaa vikosi vyake kwa ajili ya mapigano ya kukata na shoka.


Ilipofika mwaka 1961 wakati vita imekolea Marekani kwa kutumia taarifa za kijasusi ilizokusanya ilipeleka kikosi maalumu cha makomando wa Jeshi la Anga maarufu kama Green Berets kwa kazi kuu ya kufanya operations za kimya kimya za anga ili kulidhoofisha jeshi la Vietnam Kaskazini.

Kikosi hiki kiliungana baadaye na kikosi cha makomando wa anga waliojulikana kama ECO 31 na US Marines.

Tutaendelea na makala hii 

Wakati mwingine...



Kuna Humberge to kill

Hunting to kill

Full metal jacket

Phantom soldiers

Escape fo no where

Platoon of the deaths

Soldier boys 

Casualties of war 









......

Comments

Popular Posts