Historia Ya Rambo Yenye kusisimua na Fundisho Kubwa Katika Maisha yetu

 Historia Ya Rambo Yenye kusisimua na Fundisho Kubwa Katika Maisha yetu 


Sylvester Gardenzio Stallone[1] (amezaliwa tar. 6 Julai 1946), amepewa jina la utani kama Sly Stallone


6 Julai 1946 (umri 72)

New York, Marekani

Kazi yake  Mwigizaji, Mwongozaji, Mtunzi

Miaka ya kazi  1970–mpaka sasa

Ndoa  Sasha Czack (1974–1985)

Brigitte Nielsen (1985–1987)

Jennifer Flavin (1997–mpaka sasa) 


Kipindi cha nyuma, Stallone alikuwa mpambanaji kwenye maisha yake ambaye kila siku alitamani sana kuwa muigizaji mwenye jina kubwa nchini Marekani.


 Alipokuwa akiishi na mkewe, kuna siku alimuibia mke wake vito vya dhahabu na kisha kwenda kuviuza, waligombana mno mpaka kuachana. Maisha yake kwa ujumla yalikuwa magumu na mwisho wa siku akajikuta akiwa mtu asiyekuwa na mbele wa nyuma, hata pa kulala pia hakuwa napo.


Hakuwa na pa kuishi, alilala katika kituo cha mabasi jijini New York kwa siku tatu mfululizo. Hakuwa na fedha, hivyo hakuweza kulipia kodi wala kununua chakula.

 Baadae alipoona maisha magumu, akaamua kumuuza mbwa wake katika duka moja la pombe kali, alikuwa ndani huku akisubiri mteja, yeyote atakayeingia ndani na kumhitaji mbwa yule, angemuuzia.

 Sababu kubwa ya kumuuza mbwa huyo ni kwamba hata hela ya kumnunulia chakula, hakuwa nayo kabisa. Baadae akafanikiwa kumuuza kwa dola 25 tu, alipopewa fedha, akaondoka huku akilia kwani bado alimpenda mno mbwa wake, ila kwa sababu ya umasikini, hakuwa na jinsi.


Baada ya wiki mbili akaona mpambano wa ngumi kati ya Mohammed Ali na Chuck Wepner, kila alipokuwa akiiangalia ule mpambano, akajikuta akishikwa na hali ya kutaka kuandika script kwa muvi aliyoipa jina la ROCKY.


Aliandika script kwa masaa ishirini bila kulala. Alipomaliza, akataka kuiuza, watu walipoona ni nzuri, wakataka kuinunua kwa dola laki moja na ishirini na tano (zaidi ya shilingi milioni mia moja na hamsini).


 Kabla hajaiuza, akawapa wanunuaji wale ombi lake moja kwamba kama wanaitaka, basi na yeye aigize, tena awe mhusika mkuu (Starling) ambaye humo alimpa jina la ROCKY. Studio wakasema hapana, walikuwa wakimhitaji muigizaji maarufu ili wauze.


Walimwambia kwamba hakustahili kuigiza kwa kuwa alionekana kama mchekeshaji na mwenye kuchekesha sana, akawaambia kama walikataa basi anaondoka, akaondoka kweli kwenda mtaani kutafuta maisha.


Baada ya wiki chache, akaitwa tena, studio ikamwambia kwamba ingempa dola laki mbili na nusu kwa ajili ya script. Akakataa. Walimpandishia dau mpaka dola laki tatu na nusu, bado aliendelea kukataa. Wakamwambia walichokuwa wakikihitaji ni filamu yake na si yeye, naye akasema bila kuigiza mhusika mkuu kwenye muvi, hawauzii.


 Baada ya kipindi fulani, studio ikakubali, ikampa dola elfu thelathini na tano kwa ajili ya script na kumuacha naye aigize kama ROCKY ambaye ndiye mhusika mkuu kwenye hiyo filamu.


Filamu ilipotoka, ikashinda kama muvi bora ya mwaka, muongozaji wake akapokea tuzo za Oscar kama muongozaji bora na pia kuwa filamu iliyoandikwa vizuri. Hata yeye Stallone, alichaguliwa kuwania tuzo ya muigizaji bora. Mbali na hiyo, filamu hiyo ikaingizwa filamu bora za kipindi chote nchini Marekani.

 Unajua alifanya nini alipolipwa dola elfu thelathini na tano baada ya kuuza ile script? 


Stallone alimpenda sana mbwa wake, kitu cha kwanza kabisa, akataka kumnunua tena, akaenda katika lile duka la pombe kali, akaanza kumusubiri yule jamaa aliyemuuzia mbwa, alisubiri kwa siku tatu


Katika siku ya tatu, akafanikiwa kumuona jamaa aliyemuuzia mbwa akija dukani hapo huku akiwa na mbwa huyo, alichokifanya Stallone ni kuanza kumuelezea jamaa sababu iliyomfanya kumuuza yule mbwa kwamba ni ugumu wa maisha, ila katika kipindi hicho, alimhitaji mbwa wake, amnunue kwa gharama yoyote ile. Jamaa akakataa kumuuza. Stallone akampa jamaa dola mia moja. Jamaa akakataa. Akampa dola mia mbili na hamsini. Jamaa akakataa. Akampa dola mia tano. Jamaa akakataa. Akaamua kumpa dola elfu moja. Jamaa akakataa.


 Amini usiamini, Stallone alimnunua mbwa wake kwa dola elfu kumi na tano huku yeye akiwa amemuuza kipindi cha nyuma kwa dola ishirini na tano tu. Akamchukua mbwa wake na kuondoka naye.


Leo hii, Stallone yuleyule aliyekuwa akilala mitaani na kumuuza mbwa wake kwa sababu tu hakuweza kumnunulia chakula, ni mmoja wa waigizaji wakubwa, wenye fedha nyingi hapa duniani.

Kuvunjika moyo ni kitu KIBAYA. Ulishawahi kuwa na ndoto nzuri? Ndoto iliyokuhamasisha kutimiza ndoto zako lakini baadae ukavunjika moyo na kuona hutaweza? Ndugu zangu, wengi wenye mafanikio wamepitia hukohuko.


Watu watakufuata na kutaka kukatisha ndoto zako, usikubali, pambana, amini kwamba kuna siku utashinda na kuwa bora duniani, utakuwa na heshima na kila mtu atatamani kufika pale ulipofika, cha msingi, mtegemee, Mwenyezi Mungu ndio muweza wa kila kitu.

Mwaandaaji /ni Victor Oredi. 

Nalibwini



Comments

Popular Posts